MASHEIKH WA TABLIGH WA MKOA WA DAR ES SALAAM, WAITISHA MKUTANO MKUBWA KWA MASHIA WA MKOA WA DAR ES SALAAM NA PEMBEZONI MWAKE.



Maulana Hemed Jalala, Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), iliyopo Kigogo post Jijini Dar es Salaam, amewataka Mashia wa Afrika kuitambua nafasi yao katika Uislamu hususani Mashia wa Tanzania, amesema katika kikao kilichoitishwa na Masheikh wa Tabligh wa Mkoa wa Dar es Salaam, siku ya J.pili ya Tarehe 17/6/2012,Masjid Khadiir Kigogo post, jijini Dar es Salaam, pia ameongezea kwa kusema kuwa Mashia wa Tanzania wanaweza kuleta Mabadiliko ya Uchumi, Elimu, Siasa,Afya nakuendelea endapo watajitambua nafasi yao waliokua nayo kama Mashia wa Tanzania,amemalizia kwa kusema kuwa jamii yoyote ambayo haijitambui jamii hiyo itakua sawa na jamii maiti haiwezi kuleta mabadiliko yoyote katika jamii.