SAFARI YA TABLIGH MKOANI TANGA


Ziara ya Masheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam ya Tabligh imemalizika J.Pili ya Tarehe 13/5/2012 ambapo Masheikh wameweza kutembelea Madrasa katika vitongoji vya Kigombe bweni wilayani pangani kuswali na kuzungumza na Waislamu wilayani Muheza pia wamehudhuria Majils ya Bibi Fatma Zahra nakuweza kuzungumza kwenye Msikiti wa Muasasa Ahlul-Bayt (A.s), barabara ya 20 na Hawzat Qaim ya Bilal pia wametembelea Radio Maarifa msafara ukiongozwa na Maulana Hemed Jalala Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (A.s), wengine ni Shk Ghawth, Shk Muhammed Abdu, Shk Marjed, Shk Kasim, Shk Kiiza, Shk Hyder, Shk Hemed Lubumba, Shk Juma, Shk Mwamba, Shk Shukuru , Shk Said, Shk Mvuma, Shk Ramadhan, Shk Rashid, Ust Jerad Shk Hoza, Shk Mputa, takribani Masheikh na Wanaharakati 27 Ziara nyingine za Tabligh mwizi ujao wa jun na Julay zitakuwa Miono Bagamoyo, Lushoto mjini, Newala mkoani lindi Madhumuni ya Ziara hizi za Mikoani ni kwanza kujieleza sisi kama Mashia Pili kuwaeleza watu Madhebu ya Ahlul-Bayt (A.s).