Uislaamu umesisitiza zaidi kuwatendea wema wazazi wawili: "Na Mola wako ameamuru kuwa msimwabudu (yeyote) ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usiwaambie: AKH! Wala usiwakemee na sema nao kwa msemo wa heshima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma, na useme: Mola wangu! Warehemu kama walivyonilea utotoni." Qur'an 17:23-24.
Na Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) ametilia mkazo sana Mama atendewe wema zaidi kuliko Baba!
Mtu mmoja alikuja kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) akamuuliza: Kisha nani? Mtume akasema: Mama yako. Akauliza: Kisha nani? MAMA yako. Akauliza: Kisha nani? Mtume akasema: Baba yako."
Taz:
Tafsirul Qurtubi J.10 Uk. 239
Addurrul Manthur J.4 Uk. 312