Wananchi wa Nigeria wameandamana na kutoa wito wa 
kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu
 ya nchi hiyo.
Kanali ya Press TV inaripoti 
kwamba, wakazi wa mji wa Abuja nchini Nigeria jana walifanya 
maandamano, ambapo mbali na kulalamikia vitendo vya utumiaji mabavu na 
mashinikizo ya serikali dhidi ya Waislamu wametaka kuachiliwa huru mara 
moja, Sheikh Ibrahim Zakzaky anayeshikiliwa kizuizini kwa miezi kadhaa 
sasa.
Waandamanaji hao walisikika wakipiga 
nara za kukemea vikali utumiaji mabavu na mauaji ya vikosi vya usalama 
vya Nigeria dhidi ya Waislamu katika mji wa Zaria miezi kadhaa 
iliyopita.
Maandamano ya kutaka kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Waandamanaji hao wametia saini barua ambayo wameituma kwa Kamisheni ya Taifa ya Haki za Binadamu nchini humo wakitaka kuachiliwa huru mwanazuoni huyo wa Kiislamu.
Ripoti zinasema kuwa, hali ya kiafya ya 
Sheikh Ibrahim Zakzaky kizuizini ni mbaya. Pamoja na hayo, serikali ya 
Nigeria imekataa kumuachilia huru alimu huyo wa Kiislamu.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, jicho la
 kushoto  la Sheikh Zakzaky limepofuka na kwamba maafisa usalama 
wamekuwa wakikataa mwanazuoni huyo wa Kiislamu kupatiwa matibabu.
Wananchi wa Nigeria wamekuwa wakiandamana katika miji mbalimbali ya 
nchi hiyo wakitaka kuachiwa huru haraka kiongozi huyo wa Kiislamu.Jeshi la Nigeria lilipowashambulia Waislamu mjini Zaria Disemba 2015
Itakumbukwa kuwa Disemba mwaka jana askari wa jeshi la Nigeria walishambulia marasimu ya kidini ya Waislamu wa Kishia katika mji wa Zaria kwa kuwatuhumu kuwa walizuia msafara wa mkuu wa jeshi na pia kujaribu kumuua, madai ambayo yalikanushwa na Waislamu hao. (parstoda)


