TUKIO LA ISRAA NA MIRAJ SOMO LA UMOJA KWA WAISLAMU.




Mwenyekiti wa Taasisi ya Safina humanitarian and development Africa Sheikh Rajab Kiza Mussa amesema tukio la Isra na Miraji inafundisha na kuwataka Waislam kuwa na Umoja.
Sheikh Kiza aliyasema hayo jana katika Sherehe za kumbukumbu ya tukio la Isra na Miraji la Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika Msikiti Ahlulbait (a.s), upo MADALE kitongoji cha KAZA ROHO hapa Dar es salaam.
"UMUHIMU WA UMOJA KATIKA UISLAMU: Katika maajabu aliyo yaona mtume, ni Malaika aliekua nusu ya muili wake ni moto na nusu nyingine ni barafu, moto hauyayushi barafu wala barafu haizimi moto muda wote anaomba dua akisema "Ewe Mwenyezi Mungu ulie patanisha moto na barafu katika muili wangu zipatanishe nyoyo za waja wako waumini" amesema Sheikh Kiza
Aidha Sheikh Kiza amesena kuwa tukio la Isra na Miraji linafundisha Umuhimu wa Kusafiri safari za Kimasomo katika Uislam ambapo Mwislam anatakuwa asome kwa jina la Mwenyezimungu.
" Ambapo kielelezo kikuu ni safari ya Israa (kutoka Maka hadi Palestina) na safari ya Miraji (kutoka Palestina hadi Sidratul Muntaha) katika safari hii Mtume alifundishwa mambo mengi sana ikiwemo kuyaenzi maeneo matukufu, pia Mwenyezi Mungu amehimiza tusafiri kimasomo". amesema Sheikh Kiza
"Sema, tembeeni katika Aridhi kisha angalieni ulikua namna gani mwisho wa wakadhibishao" (AN'AAM:11).