JITIHADA ZA KUUNG'OA MFUMO WA WILAYAH KATIKA ZAMA ZETU.

Ukombozi wetu upo chini ya Mfumo wa Wilayah leo hii maadui na wanyang'anyi wameona njia pekee ya kuwafanya watu dhahifu ni kuwapokonya mfumo huu wa Wilayah ili wasiweze kupata muelekeo katika kusimamia baadhi ya mambo.

Matatizo yaliko ndani ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran baada ya Mapinduzi ya Kiislam yenyewe ni somo tosha; tena yote haya yanahusika kwenye ukweli kwamba Mapinduzi ya Kiislam yalolenga na kuweka juhudi katika kutekeleza Mfumo wa Wilaya. Ni lazima idhihirike kwetu sisi kuhusu njama za mipango ya maadui wa Mapinduzi na dini, zile mamlaka zenye kiburi zilizonayo juu ya Iran; na wanashughulika kivitendo juu ya mipango hii. Kama unavyoweza kuona baadhi ya mambo kwa uwazi kabisa, kuna uingiaji mkubwa wa bajeti ya Kimarekani kwa ajili ya kueneza uharibifu wa tamaduni miongoni mwa watu, na hilo nalo hususani ni kwa vijana. Mamilioni ya dola za Kimarekani yanasambazwa ili kuwavuruga vijana wa Iran na kuwachochea dhidi ya Mfumo wa Wilayah, kuwaingiza wanawake wa Kiirani kwenye utovu wa staha na upujufu, kuwafanya vijana wa Iran kuwa waathirika wa madawa ya kulevya, kueneza maelezo ya matusi ya kingono na lugha chafu; yote haya yanafanywa na bajeti ya baraza la Congress la Marekani mahususi na iliyotamkwa wazi hadharani kwa ajili ya opresheni za siri siri ndani ya Iran. Mbali na hii, bajeti isiyotamkwa hadharani ni kubwa zaidi kuliko ile iliyotamkwa katika kueneza mmomonyoko wa maadili ndani ya Iran. Na Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi