Kiongozi
wa Chuo Kikuu cha al-Azhar nchini Misri Ahmad al-Tayib, ametaka kuundwe
kikosi maalumu cha nchi za Kiarabu kitakachokuwa na jukumu la
kukabiliana na makundi ya kigaidi. Ahmad al-Tayib ameyasema hayo katika
sherehe za kufunguliwa kongamano la 24 la kimataifa la Baraza Kuu la
Mambo ya Kiislamu na kuongeza kuwa, ugaidi unaoendelea ndani ya nchi za
Kiarabu, hauwezi kuangamizwa kinyume na majeshi yasiyo ya Kiarabu. Kiongozi
wa Chuo Kikuu cha al-Azhar nchini Misri amesisitiza kwamba, katika
kumaliza makundi ya magaidi, Waarabu wanatakiwa kubeba silaha na
kuzielekeza kwa makundi hayo. Aidha amesisitiza juu ya udharura wa
kuyaunganisha pamoja majeshi hayo ya Kiarabu kwenye jeshi la serikali ya
Misri ili kufanikisha kung'oa mizizi ya makundi ya kigaidi. Kabla ya
hapo pia Rais Abd Al- Fattah al Sisi wa Misri alitoa pendekezo la
kuundwa kikosi cha nchi za Kiarabu kwa ajili ya kukabiliana na ugaidi.
Hivi karibuni pia Sheikh Ahmad al-Tayib, alitoa mwito kwa nchi za
Kiislamu kufanyia marekebisho mitalaa ya elimu katika taasisi za elimu
ili kupunguza wimbi la vijana kujiunga na makundi ya kigaidi duniani.
Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/47029-al-azhar-kuwepo-jeshi-la-k…