Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa
kuongezwa juhudi za kukabiliana na changamoto zinazoukabili ulimwengu wa
Kiislamu.
Dakta Ali Larijani amesema hayo leo kabla ya kuondoka Tehran na kuelekea Uturuki kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa Muungano wa Mabunge ya Nchi za Kiislamu na kusisitiza kwamba, miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni changamoto zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu na namna ya kuzipatia ufumbuzi.
Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu ya Iran amebainisha kwamba, hii leo nchi za Kiislamu zinakabiliwa na changamoto ambazo zimepelekea kuhatarisha usalama wa Mashariki ya Kati na kujitokeza masuala kama ya ugaidi. Mkutano wa siku tatu wa Muungano wa Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC unaanza kesho nchini Uturuki.
Akiwa nchini Uturuki, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo pia na maspika mbalimbali wa mabunge ya Kiislamu na kubadilishana nao mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya kieneo na kimataifa likiwemo suala la shambulio la hivi karibuni la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya muqawama huko nchini Syria, shambulio ambalo lilipelekea kuuawa shahidi wanachama sita wa Hizbullah akiwemo mtoto wa shahidi Emad Mughniya.
DK. LARIJANI: MUQAWAMA UNAPASA KUIMARISHWA ZAIDI.
Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, misingi ya muqawama inapaswa kuimarishwa zaidi kwa kuwepo umoja na mshikamano zaidi kwa wanamapambano wa Palestina, Syria na Lebanon. Dakta Ali Larijani ameyasema hayo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Ahmad Jibril Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina na kusisitiza kwamba, ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kulitilia umuhimu suala la kukombolewa ardhi za Palestina.
Spika Larijani ameongeza kuwa, sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa bega kwa bega na wananchi wa Palestina na kuwaunga mkono kwa hali na mali katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel. Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu amezikosoa vikali baadhi ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati kwa kuyasaidia madola ya Magharibi na kubainisha kwamba inasikitisha kuona kwamba baadhi ya nchi za Kiarabu za eneo kwa kushirikiana na madola ya Magharibi zimefanya njama za kupunguza bei ya mafuta, kwa lengo la kuendeleza sera zao za kutaka kujitanua zaidi na zilizo dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu.
Kwenye mazungumzo hayo, naye Ahmad Jibril ameusifu msimamo wa Iran wa kuwasaidia wananchi wa Palestina kwa lengo la kuikomboa Quds Tukufu' Kibla cha kwanza cha Waislamu' na kusisitiza kwamba wananchi wa Palestina kamwe hawatasahau misaada inayotolewa na wananchi na taifa la Iran kwa wananchi wa Palestina. Katibu Mkuu wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina ameelezea matukio yanayoendelea kushuhudiwa huko Syria na Iraq kuwa ni njama za madola ya kibeberu za kutaka kuusambaratisha muqawama na kusisitiza kwamba njama hizo zinapaswa kuzimwa.
WANACHUONI IRAN WALAANI KUVUNJIWA HESHIMA MTUME (S.A.W).
Maelfu ya wanafunzi na wanazuoni wa Vyuo Vikuu Vya Kiislamu Katika mji wa Qum, Iran wamefanya maandamano makubwa wakipinga kitendo cha gazeti la Charlie Hebdo la nchini Ufaransa kuchapisha vikatuni vya kumvunjia heshima Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Maandamano hayo yaliyofanyika katika chuo cha Faidhiya cha mjini Qum, yamewashirikisha wanafunzi , wahadhiri na wanazuoni kutoka nchi mbalimbali za dunia kulaani kitendo hicho cha kumvunjiwa heshima Mtukufu Mtume (SAW). Katika maandamano hayo, waandamanaji walitoa nara za kulaani gazeti hilo kwa hatua ya kuthubutu kuchezea hisia za Waislamu zaidi ya bilioni mbili duniani. Hujjatul-Islam Wal-Muslimin, Sayyid Muhammad Saidi, ambaye pia ni msimamizi wa Haram ya Bibi Fatima Maasumah, kwa kusema: "Maadui wa Uislamu wamefuata mkondo huo baada ya wao kushindwa kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu yaani Uislamu na kwamba hiyo ni juhudi iliyofeli." Jana pia maelfu ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran waliandamana mbele ya Ubalozi wa Ufaransa mjini Tehran kulaani hatua ya gazeti la Charlie Hebdo kuchapisha tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume wa Uislamu Muhammad (SAW). Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/46055-wanachuo-iran-walaani-kuvu…