(Waumini wa Kiislam nchini Ghana)
TUKIO LA GHADIR KHOM: "Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako, na kama hukufanya, basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu, hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri." (Qur'an: 5:67) Tarehe kumi na nane mwaka wa kumi Hijria, majira ya Asubuhi, Mtume (s.a.w.w) alipokuwa akirejea kutoka Makka baada ya kufanya ibada ya Hijjah, akiandamana na Waislam zaidi ya laki moja. Mtume (s.a.w.w) pamoja na Waislam walipofika njia panda, njia ziendazo Madina, Misri na Iraq, katika bonde la Khom, ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya: "Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako, na kama hukufanya, basi hukufikisha ujumbe wake." Mtume (s.a.w.w) akashika mkono wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) akasema: "Ambaye mimi natawalia mambo yake, basi Ali ni mtawala wake. Ee Mwenyezi Mungu! Muunge atakayemuunga na mtenge atakayemtenga (Ali) mnusuru atakayemnusuru, mtupe atakayemtupa (Ali)." kisha baada ya hapo, Maswahaba walianza kutoa kiapo cha utiifu kwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) kama tunavyomnukuu hapa Umar bin Khattab: "Hongera ewe mwana wa Abu Talib, umekuwa kiongozi wangu na kiongozi wa Waislam wote." Rejea: Tafsirun Naysabury J. 6 Uk. 194, Tarekh Bughdad J. 8 Uk. 290, Tafsirul Kabiir J. 12 Uk. 49. pale pale Mwenyezi Mungu akateremsha Aya: "Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema yangu, na nimewapendeleeni Uislam uwe dini yenu." (Qur'an: 5:3) Rejea: Tarekh Bughdad: J. 8 Uk. 290, Tarekh Ibn A'sakir: J. 2 Uk. 75.