KERMANI: HUKUMU YA KIFO DHIDI YA SHEIKH NIMRI SIO HALALI.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ameionya Saudia Arabia kuhusiana na hukumu ya kifo dhidi ya mwanazuoni mashuhuri wa Kishia nchini humo Ayatullah Sheikh Nimr Baqir al-Nimr.
Ayatullah Muhammad Ali Movahhedi Kermani amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini katika ibada ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kusisitiza kwamba, hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya Sheikh Nimr sio halali. Amesema kuwa, kutolewa hukumu ya kifo dhidi ya Sheikh Nimr kutakuwa na matokeo mabaya mno kwa serikali ya Saudia hasa kwa kutilia maanani kwamba, theluthi moja ya wakazi wa nchi hiyo ni Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa hapa Tehran ameashiria jina za kundi la kigaidi la Daesh huko Iraq na Syria na kusema kuwa, jambo lililo wazi ni kwamba, Marekani kwa kutumia vibaya muungano eti dhidi ya Daesh, inataka kujiandalia uwanja wa kuwepo tena kijeshi Iraq na kwa upande wa Syria iangamize miundo mbinu ya nchi hiyo.
Kuhusiana na kuwadia mwezi wa Muharram unaoanza kesho, Sheikh Movahhedi Kermani amesisitiza umuhimu wa kufanya maombolezo ya Imam Hussein (as) mjukumu wa Mtume (saw) na kubainisha kwamba, harakati ya Imam Hussein pamoja na masaibu aliyokumbana nayo yeye pamoja na wafuasi wake ni jambo linaloonesha kwamba, wakati mwingine mwanadamu anapaswa kuvumilia machungu na masaibu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.Chanzo cha habari:
http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/43976-ayatullah-kermani-hukumu-ya-kifo-dhidi-ya-sheikh-nimri-sio-halali