JA'FARI: TANZANIA NI LANGO LA KUINGIA AFRIKA MASHARIKI.

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amesema kuwa, Tanzania ni lango la kuingizia bidhaa za Kiirani katika eneo la Afrika Mashariki.
Balozi Mehdi Agha Ja'fari amezungumzia uwanja wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi muhimu mno kwa ajili ya kusafirisha na kupeleka nje bidhaa za Iran zis
izo za mafuta na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa lango la kuingiza bidhaa za Kiirani huko Afrika Mashariki.
Balozi Mehdi Agha Ja'fari amesema, Tanzania na bandari ya Dar es Salaam kuwa pambizoni mwa bahari ya Hindi na kuwa kwake karibu na maeneo ya kiuchumi ya magharibi mwa Asia hususan Ghuba ya Uajemi ni sifa nzuri zinazotayarisha mazingira bora ya kufanyika biashara kati ya Tanzania na Iran. Balozi wa Iran mjini Dar es Salaam amesema kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa, usafirishaji wa bidhaa zisizo za mafuta za Iran kuelekea Tanzania umeongezeka mno katika kipindi cha miaka minne ya hivi karibuni. Chanzo cha habari
: http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/43972-ja-fari-tanzania-ni-lango-la-kuingia-afrika-mashariki