Mwaka 1994 mimi niliamua kuwa Shia Ithna 
Asharriyah na wenyeji wangu walionipokea ni Bilal Muslim Mission of 
Tanzania chini ya uongozi wa Maulana Akhtar Rizivi na utendaji wa Mzee 
Fidah Husain Hameer. Ombi langu la kwanza kwao ili niwe Mwanaharakati
 mzuri wa Madhehebu ya Ahlul Bayt (a.s) nijengewe Msikiti mjini Lushoto 
ambapo ndipo mimi kwa miaka karibu 15 nilifanikiwa kueneza 
Uwahhabi(Answaru Sunna) Wilaya yote ya Lushoto. Na nilifanikiwa kujenga 
misikiti isiopungua 10 chini ya African Muslim Agency. Mimi nilikuwa 
msitari wa mbele katika mapambano na madhehebu ya Sunni (Madhehebu ya 
Shafii) ambayo ndio yaliyokuwa Wilaya ya Lushoto na Tanga yote kwa 
jumla. Katika Tanzania yote kwa ujumla chini ya vijana wa Warsha ya 
Waandishi wa Kiislamu tulifanikisha kuanzisha Seminari za Kiislamu, 
nikiwa Kiongozi wa Idara ya D’awa, nilisimama mahakamani mwaka mzima kwa
 niaba ya Warsha ya Waandishi wa Kiislamu kuishitaki Wizara ya Elimu na 
BAKWATA kwa kuwanyima Waislamu wasiwe na Seminari zao wakati Wakristo 
wanazo. Kesi hiyo tulishinda na Masjid Qubah ikiwa Seminari ya kwanza 
Tanzania bila kuwa chini ya BAKWATA. Ushindi wa kesi hiyo ukafungua 
milango kwa Waislamu wakawa na Seminari zao. Almuntaziri ikiwa moja 
wapo. Kwa msingi huo tulikubaliana tujenge msikiti Lushoto mjini lakini 
kiwanja kiwe kwa jina la Rejesterd Trustees of Bilal Muslim Mission of 
Tanzania. Mimi nilitafuta kiwanja baada ya kukosa nilikubali kutoa 
kiwanja changu kilichoko mjini Lushoto (Wakfu) kwa Bilal Muslim Mission 
of Tanzania ili mradi tuwe na msikiti mjini. Insha’allah tutaendelea 
kuwapatia historia ya Mwanaharakati huyu mkongwe
