Hii inatuonyesha ya kuwa Udhalili hautakiwi
kwa Mwanadamu kwa kuhofia vikwazo na vitisho kutoka kwa wenye nguvu,
mwanadamu anatakiwa kusimama imara siku zote katika kupambana na dhulma,
ukandamizaji pamoja na unyanyasaji dhidi ya mwanadamu kukaa
kimya ni sawa na kuunga mkono dhulma . Hapa ni muhimu sana tukumbuke
maneno ya mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alipotoka pamoja na familia
yake na Masahaba zake kuelekea katika ardhi ya Karbala kwa ajili ya
kujitolea Muhanga maisha yao kwa ajili ya kuchunga heshima na Utukufu
wa mwanadamu. Imam Hussein (a.s) alisema: "Daima udhalili ni mwiko
kwetu"