Waumini wa dini ya kiislam leo wamefanya Sherehe ya kusherehekea mazazi ya kuzaliwa Bint wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), Sherehe hiyo imefanyika Masjid Al-Ghadiir, jijini Dar es Salaam chini ya uongozi wa Maulana Sheikh Hemed Jalala, katika Sherehe hiyo kulipambwa na Mashairi pamoja na Qaswida za kumsifu bint huyo Mtukufu na kiunganishi kati ya Uimamu na Utume.