MAREKANI YALAANIWA KWA KUMZUIA BALOZI WA IRAN UN.



Mbunge wa ngazi za juu nchini Iran amelaani vikali uamuzi wa Marekani kumnyima visa balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu katika Umoja wa Mataifa.
SIku ya Jumamosi, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Bunge la Iran Alaeddin Boroujerdi alisema, ' kutokana na kuwa Hamid Aboutalebi amechaguliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Matiafa , taasisi ambayo makao yake makuu yako ndani ya ardhi ya Marekani, hatua ya wakuu wa Marekani kumnyima visa Aboutalebi ni sawa na kutumia vibaya eneo la kijiografia la Umoja wa Mataifa.'
Marekani imeamua kumnyima visa Aboutalebi kutokana na kuwa alihusika katika kuuteka ubalozi wa Marekani mjini Tehrna katika matukio  ya baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979.
Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Marekani kama mwenyeji wa makao makuu ya Umoja wa Mataifa inapaswa kutoa visa kwa wawakilishi wa nchi wanachama wa umoja huo pasina kuweka vizingiti.



WAZAYUNI WANAJISI KIBLA CHA KWANZA CHA WAISLAMU:


Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kwa mara nyingine tena wamewashambulia raia wa Palestina katika uwanja wa msikiti mtakatifu wa al Aqswa katika mji mtakatifu wa Quds.
Ghasia hizozilizuka leo wakati polisi walipowazuia Waislamu kuingia katika moja ya milango ya msikiti huo.
Wanajeshi wa utawala haramu wa Kizayuni walirusha maguruneti ili kuwatawanya waandamanaji wa Kipalestina.
Itakumbukwa kuwa wanajeshi wa Israel na walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali katika miezi ya hivi karibuni wamezidisha mashambulizi yao dhidi ya Wapalestina wanaoingia katika msikiti wa al Aqswa.
Mashambulizi hayo yamesababisha kuzuka mapambano makali kati ya Wapalestina na wanajeshi katili wa Israel.
Mbali na kuwashambuliwa raia wa Palestina, Utawala wa Kizayuni wa Israel umeweka pia vizuizi vikali ili kuwazuia Waislamu kuingia msikitini humo. Itakumbukwa kuwa msikiti wa al Aqswa ndicho kibla cha kwanza cha Waislamu kabla ya al Kaaba. 

 Imam Khomein alikuwa Muislamu wa Madhehebu ya Shia ambaye alikuwa akiamini sana udharura wa kuwepo umoja wa Ummah wa Kiislamu (bila ya kujali mielekeo yao ya Kimadhehebu) katika kukabiliana na wakoloni na maadui wa Uislamu. Wito wa kuwepo umoja na mshikamano umechukua sehemu kubwa ya ujumbe na hotuba za Imam. Imam alikuwa akiharamisha na kukataza harakati yeyote inayozusha hitilafu katika safu za Waislamu na kuwatayarishia wakoloni fursa ya kuwatawala. Alibaini njia ya kivitendo ya umoja kati ya Waislamu wa Shia na Sunni kwa kutoa fatuwa ya kipekee katika uwanja huo na kutangaza “Wiki ya Umoja” katika ulimwengu wa Kiislamu, na kukumbuka siku ya kuzaliwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w). katika kipindi chote cha uongozi wake, Imam alisimama kidete kukabiliana na njama zote za kuzusha hitilafu na mfarakano kati ya Shia na Sunni. Imam Khomein aliamini kwamba, imani ya Mwenyezi Mungu mmoja, utume wa Mtume wa mwisho (s.a.w.w), Qur’an Tukufu, ambacho ni kitabu cha milele cha uongofu, na pia itikadi ya masuala ya dharura na sharia za dini kama vile Swala, Funga, Zakka, Hijja na Jihadi, ni misingi imara ya umoja wa kivitendo wa wafuasi wa Madhehebu zote za Kiislamu katika kukabiliana na washirikina na maadui wa dini.