SAYYID HASSAN NASRALLAH: MAREKANI IMETENDA JINAI NYINGI.


Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa serikali ya Marekani imeanzisha vita vingi na kutenda unyama mkubwa duniani. Sayyid Hassan Nasrullah ameongeza kuwa, moja kati ya jinai kubwa zilizotendwa na Wamarekani ni mashambulio ya nyuklia kwenye miji ya Hiroshima na Nagasaki nchini Japan.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameashiria matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei aliyesema hivi karibuni kwamba ubalozi wa Marekani mjini Tehran ulikuwa pango la kijasusi na kusisitiza kuwa, balozi zote za Marekani duniani ni mapango ya ujasusi.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameongeza kuwa kila mwaka ndege zisizo na rubani za Marekani zimekuwa zikiuwa maelfu ya watu wasio na hatia na hakuna mtu au taasisi yoyote inayopaza sauti ya kufunguliwa mashtaka viongozi wa nchi hiyo kwa kutenda jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu.