HIZBULLAH YAWATAKA WALEBANON WAJIHADHARI NA FITINA.


Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amewataka wananchi wa nchi hiyo wajiweke mbali na fitina na kuwa tayari kukabiliana nayo.

Sheikh Naim Qassim
amesisitiza juu ya udharura wa kujiweka mbali na fitina na wakati huo huo kusimama na kukabiliana nayo. Amesema, ili kukabiliana na fitina kuna haja ya kuzingatiwa mambo matatu ambayo ni kujiweka mbali na uchochezi wa kimadhehebu, kujiepusha kuchukua misimamo ya kimadhehebu na kutoruhusu mazungumzo baina ya pande mbalimbali kusitishwa.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza pia juu ya ulazima wa kuundwa serikali mpya ya Lebanon haraka iwezekanavyo na hivyo kuifanya nchi hiyo isishindwe kukabiliana na migogoro. Sheikh Naim Qassim amesema bayana kwamba, kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Lebanon ndio njia pekee ya kuikwamua nchi hiyo na matatizo inayokabiliwa nayo. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/33816-hizbullah-yawataka-walebanoni-wajihadhari-na-fitina