Kitengo cha kusimamia vitendo vya kiadui dhidi ya dini ya Kiislamu (Islamophobia) katika Baraza la Utamaduni la Waislamu nchini Ufaransa kimeeleza juu ya ongezeko kubwa la vitisho dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu nchini humo. Gazeti la Le Monde linalochapishwa nchini Ufaransa limechapisha ripoti iliyotolewa na kitengo hicho na kueleza kuwa, vitisho na uadui dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu vimeongezeka mno katika kipindi cha miezi sita ya awali ya mwaka 2013, ikilinganishwa na kipindi hichochicho mwaka 2012. Abdallah Zekri mkuu wa kitengo hicho amesema kuwa, vitendo vya ukandamizaji na udhalilishaji dhidi ya Waislamu vimefikia 108, ikilinganishwa na matukio 80 yaliyojiri mwaka 2012 katika kipindi cha miezi sita ya awali. Zekri ameongeza kuwa, vitisho na vitendo vya utumiaji nguvu kwa kipindi cha miezi sita ya awali katika mwaka 2012 vilikuwa 63, na mwaka huu wa 2013 vimefikia 84, ikiwa ni ongezeko la asilimia 33. Ukiangalia kwa makini takwimu hizo tunaona kwamba katika kipindi cha miezi sita ya awali ya mwaka huu, vitendo vya chuki na uadui dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa vimeongezeka kwa asilimia 35 ikilinganishwa na mwaka uliopita, na takwimu hiyo haikuzingatia baadhi ya matukio mengine ambayo hayakuripotiwa kwenye vituo husika. Abdallah Zekri kutoka Baraza la Utamaduni la Waislamu nchini Ufaransa amesisitiza kuwa, wasiwasi mkubwa uliopo ni kuwepo uvamizi dhidi ya wanawake wanaovaa hijabu ya Kiislamu nchini humo. Zekri amesisitiza kuwa, katika kipindi cha miezi mitatu tu iliyopita, wanawake watano wa Kiislamu waliokuwa wamevaa vazi la stara la Kiislamu walifungua mashtaka baada ya kuvamiwa na watu waliokuwa na chuki dhidi ya Uislamu. Wanawake hao wamesema kuwa, licha ya kushambuliwa na vijana hao waliokuwa na chuki dhidi ya Uislamu, walitupiwa maneno mengine machafu yaliyokuwa dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu na Waislamu. Matamshi hayo ya afisa mwandamizi wa Baraza la Utamaduini la Waislamu nchini Ufaransa yanatolewa katika hali ambayo, viongozi wa serikali ya Paris na wanasiasa wa Ufaransa wanakiri kuongezeka vitendo vya chuki na uadui dhidi ya dini ya Kiislamu vinavyofanywa na makundi ya mrengo wa kulia yenye misimamo ya kuchupa mipaka. Manuel Valls Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa ametoa matamshi yake ya kijuba pale alipotetea mashambulizi yanayofanywa dhidi ya wanawake wanaovaa hijabu ya Kiislamu nchini humo. Jean Marie Le Pen muasisi wa chama cha National Front chenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia, aliikosoa vikali serikali ya Paris kutokana na matukio yaliyojiri katika mji wa Trappes. Hatua ya jeshi la polisi la Ufaransa la kupambana na hata kumvunjia heshima mwanamke wa Kiislamu mbele ya mumewe katika mji wa Trappes, ilikabiliwa na ukosoaji mkubwa wa wananchi nchini humo. Vitendo hivyo vya kiadui vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku kutokana na viongozi wa serikali kunyamazia kimya unyama unaofanywa dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu nchini Ufaransa, na hasa kwa wanawake. Vitendo vya kuharibu makaburi ya Waislamu, kushambulia na kuharibu Misikiti na mbinyo uliowekwa dhidi ya wanawake wa Kiislamu wanaovaa hijabu, ni miongoni mwa vitendo vya uadui vinavyofanywa dhidi ya Waislamu nchini humo. Miaka ya hivi karibuni , viongozi wa Ufaransa walipitisha sheria mbalimbali za kidhuluma ikiwemo ile ya kuweka mbinyo dhidi ya shughuli za Waislamu na wanawake wanaovaa vazi la stara yaani hijabu. Tokea mwezi Aprili mwaka 2011, ilipitishwa sheria ya kibaguzi ambayo iliwapiga marufuku wanawake wa Kiislamu kuvaa hijabu au burqa katika maeneo ya umma na mkusanyiko ya watu, sheria ambayo imepingwa vikali na Waislamu na wananchi wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa sheria hiyo, wanawake watakaopatikana wamevaa hijabu kwenye maeneo ya umma, watakabiliwa na adhabu ya kupigwa faini ya euro 150 pamoja na kuhudhuria kwa nguvu mafunzo ya kiraia. Sheria hiyo ilipitishwa katika hali ambayo, kuna Waislamu wapatao milioni nane wanaoishi hivi sasa nchini Ufaransa. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/uchambuzi/item/33588-kuongezeka-vitendo-vya-chuki-na-uadui-dhidi-ya-dini-ya-kiislamu-nchini-ufaransa
KUONGEZEKA VITENDO VYA CHUKI NA UADUI DHIDI YA DINI YA KIISLAMU NCHINI UFARANSA.