Jana Ijumaa tarehe 14 Juni saa mbili asubuhi vituo vya kupigia kura ndani na nje ya Iran katika nchi 96 duniani vilifunguliwa, ili Wairani waweze kushiriki katika uchaguzi wa kuainisha mustakbali wa nchi yao. Hapo jana wananchi nchi nzima na nje ya nchi walielekea katika vituo vya kupigia kura ili kushiriki katika duru ya 11 ya uchaguzi wa rais uliofanyika sambamba na uchaguzi wa duru ya 4 wa mabaraza ya miji na vijiji. Uchaguzi katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran una tajriba ya umri mzima wa Mapinduzi ya Kiislamu kiasi kwamba, kwa wastani uchaguzi mmoja hufanyika nchini kila mwaka, suala linalodhihirisha wazi jinsi mwenendo wa uchaguzi unavyozidi kukomaa hapa nchini. Nukta ya kuzingatiwa kuhusiana na kufanyika kwa pamoja chaguzi mbili tarehe 14 Juni mwaka huu, ni kushuhudiwa hamasa kubwa ya kisiasa na kujitokeza kwa wingi wananchi. Kwa ajili hiyo, mahudhurio hayo makubwa yanazingatiwa sana na maadui wa mfumo wa Kiislamu hasa pale wanapojadili mustakbali wa taifa la Iran. Kwa msingi huo tukiachilia mbali suala la uchaguzi ambao matokeo yake yatajulikana baada ya kumalizika zoezi la kuhesabiwa kura, nafsi ya wananchi kujitokeza katika chaguzi zinazofuatana, linadhamini nguvu na mshikamano wa taifa la Iran, ambao ndio mtaji mkubwa wa kisiasa na kijamii, na mustakbali wa taifa hili. Kujitokeza kwa wingi na kwa ufahamu wananchi katika uchaguzi wa Ijumaa, kulikoshuhudiwa huku mashirika ya habari ya nchi za Magharibi na hata viongozi wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya wakidai kwamba hakuna uwazi katika uchaguzi na kwamba wananchi hawatoshiriki kwa wingi katika uchaguzi huo, kwa mara nyingine tena kumeonesha jinsi mitizamo ya Wamagharibi kuhusu Iran isivyokuwa sahihi. Kwa ajili hiyo tunapaswa kusema kuwa, kujitokeza kwa wingi wananchi katika uchaguzi wa mwaka huu kunatokana na masuala tofauti. Kwanza kabisa ni kuwa, wananchi wa Iran wanaamini kwamba kushiriki katika uchaguzi ni jukumu na haki yao ili kufikia matakwa yao kwa mujibu wa malengo na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu, na kila wanapohisi umuhimu wa kujitokeza, hutekeleza vizuri jukumu hilo na kwa umakini mkubwa. Suala la pili ni kuwa, uchaguzi wa duru hii ulikuwa na wagombea wenye sifa tofauti na wa mirengo mbalimbali ambapo kila mmoja aliingia katika kinyang'anyiro hicho kwa nia ya kushinda na ilikuwa vigumu kutabiri ni mgombea gani kati yao angeweza kushinda. Sula la tatu ni usalama na kuheshimiwa sheria ambako kulionekana wazi katika uchaguzi huu,jambo ambalo wachambuzi wa mambo wanasema limekuwa na nafasi muhimu katika kuandaa mazingira ya kushiriki matabaka yote ya wananchi katika uchaguzi wa wazi, huru na wa haki. Suala la mwisho lililopelekea wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye duru hii ya uchaguzi ni kukomaa na kuimarika kwa mwenendo mzima wa uchaguzi hapa nchini. Ala kullihal, uamuzi wa mwisho katika uchaguzi ni wa wananchi, ambao kwa kutumia kura zao humchagua mtu ambaye wanaona anafaa kuwaongoza.Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/uchambuzi/item/32675-uchaguzi-wa-mwaka-huu-wa-iran
UCHAGUZI WA MWAKA HUU WA IRAN.