Shirika la habari la AhlulBayt (a.s) -ABNA; Masalafia kadha siku ya juma tatu iliopita wamekusanyika katika sehemu iitwayo Abu Hilali katika mkoa wa Munyai nchini Misri na kuasisi taasisi kwalengo ya kile walichokiita kuwa kusambaa na kuenea kwa Ushia nchini Misri
Taasisi ya Kitabligh ya kufikisha ujumbe wa kupambana na Ushia ikiwa na anuani hii kwa Lugha ya kiarabu (مركزبلاغ الدعوى لمكافحة التشيع ) na kuasisi taasisi hiyo kwa lengo ya kile walicho kiita kuwa hatari ya kuenea ushia nchini humo.
Miongoni mwa malengo na ratiba za taasisi hiyo ni kutembelea mikoa na vijiji na kuweka semena tofauti nchini, pia kuzalisha video ambazo zitakuwa zinaonyesha itikadi mbaya za mashia (kwa maana ya kuwazulia mashia katika yale wasio yaamini).
Vitendo hivyo vya masalafia hao dhidi ya mshia ni katika hali ambayo kwa ujumla Misri yote kunamashia milioni moja tu wakiishi katika nchi hiyo, ama siku hadi siku wanazidi kubanwa kiasi kwamba hawana hata amani katika jamii hiyo, na hii nikatika hali ambayo mashia wa nchi hiyo wanaishi kindugu pasina kuwa na chuki za kimadhehebu mengine na kuepuka kila aina za kusababisha hitilafu baina yao na ndugu zao Masunni katika jamii hiyo lakini mashia hao bado wako na mashaka katika maisha yao.
Maulamaa wa kishia wa nchi hiyo katika kipindi chote wamekuwa wakijibu uzushi na masuala wanayo zushiwa na masalafia hao lakini mpaka sasa bila yakutoa ushahidi wa kuwahusisha na itikadi potofu bado wanazidisha kuwabana wananchi hao wachache. Habari kutoka http://www.abna.ir/data.asp?lang=17&id=428755