Rais wa baraza la kimataifa linahusiana umoja wa madhehebu ya kiislamu amesisitiza kuwa kuvunjiwa heshima matukufu ya kiislamu na harakati zinazokwendfa dhidi ya uislamu vitasababisha fitna kubwa katika ulimwengu wa kiislamu.
Ayatollah Muhammad Ali Taskhirii ameyasema hayo akiashiria vitendo ya kinyama vinavyofanywa na waasi wa serikali ya Siria, ambao wamekuwa wakifanya matendo yanayokwenda kinyume na mafunzo ya dini tukufu ya kiislamu ili hali wanajinadi kuwa ni waislamu, na baadhi ya mataifa ya kiislamu yanawaunga mkono na kuwapatia silaha na misaada mingine ili wafikie lengo lao.
waasi hao licha ya kufanya mauaji ya kinyama na ubakaji, wamevunja misikiti, athari za kiislam na makaburi ya kihistoria kama makaburi ya maswahaba, na pia wamekuwa wakiharibu mashule na asasi nyingi za kijamii.
Ayatollah Taskhirii ameendelea kusisitiza akisema: ni wadhifa kwa wanazuoni na Maulamaa wote wa kiislamu kuhakikisha wanakabiliana na vitendo hivi vya kinyama.