Mwalimu wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s),
Sheikh Said Othaman, amewahutubia Waumini wa dini ya Kiislam leo katika
Masjid Ghadiir, Kigogo Post, Da re Salaam, amewataka Waumini hao kuwa na
Umoja na Mshikamano baina yao, pia amesema Waislam hawanabudi kuyafuata
mafundisho ya Imam Ali bin Abi Talib (a.s), na kuangalia jinsi gani
alivyoweza kuishi na jamii.
Baadhi ya Waumini wakiwa katika Sherehe ya
Mazazi ya Imam Ali bin Abi Talib (a.s), iliyofanyika leo Masjid Ghadiir,
Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, Sherehe hiyo iliongozwa na Sheikh
Said Othaman Mwalimu wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), iliyopo Kigogo
Post, Dar es Salaam.
Waumini
wa Madhehebu mbalimbali ya Kiislam leo wameungana Masjid Ghadiir,
Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, kusherehekea Mazazi ya Imam
Ali bin Abi Talib (a.s), katika picha Waumini hao wakisoma Dua ya Umoja
na mshikamano baina ya Waislam.