"MAADUI WANACHOCHEA UADUI BAINA YA WAISLAMU"


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa, maadui wanataka kuwasha moto wa uadui kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni kwa kuvunjia heshima haramu tukufu ya swahaba wa Mtume SAW nchini Syria.

Akiwahutubia hii leo maafisa wanaoshughulikia uchaguzi wa duru ya 14 wa rais hapa nchini, Ayatullah Khamenei ametoa wito wa kuendelea kulaaniwa kitendo cha kuvunjiwa heshima kaburi tukufu la Sahaba wa Mtume Muhammad (SAW) Hujr bin Adi (R.A)

Ayatullah Khamenei ametahadharisha kwamba, vitendo kama hivyo vitaendelea iwapo maulamaa wa Kiislamu na shakhsia wa kisiasa watashindwa kuvikemea na kuvilaani.

Katika upande mwingine Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kujitokeza kwa wingi wananchi katika duru hii ya uchaguzi wa rais hapa nchini Iran kutaupa iitibari uchaguzi na kudhamini maendeleo na ustawi wa taifa. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/kiongozi/item/31673-maadui-wanataka-kuchochea-uadui-baina-ya-waislamu