Ofisi ya Uwakilishi ya Syria katika Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa kundi la al Nusra linaloshirikiana na mtandao wa al Qaida limekiri kutekeleza mashambulizi 6000 ya kigaidi nchini humo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Ofisi hiyo imeripoti kuwa, baadhi ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama la umoja huo zimejizuia kutoa taarifa za kulaani mashambulizi hayo ya kigaidi ya, ambayo yameuawa mamia ya raia wasio na hatia wa Syria. Saudi Arabia, Qatar, Uturuki, Marekani, Uingereza, utawala wa Kizayuni na pande nyingine za kigeni zimekuwa zikiwapa magaidi wa Syria msaada wa fedha, silaha na wa vyombo vya habari tangu mwaka juzi hadi sasa na hivyo kuitumbukiza Syria katika mchafukoge kwa shabaha ya kuung'oa madarakani uongozi wa nchi hiyo ambao ni moja ya mihimili ya muqawama dhidi ya Uzayuni katika eneo. Wakati huo huo Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Usulud-Din katika chuo Kikuu cha Al-Azhar, ameitaja hatua ya kufukua kaburi la sahaba wa Mtume (SAW) huko nchini Syria kuwa ni dhambi kubwa na uadui dhidi ya dini Tukufu ya Kiislamu. Abdur-Rahman al-Birr mkuu wa chuo kilichotajwa cha Al-Azhar ambaye pia ni mjumbe wa ofisi ya miongozo ya Harakati ya Ikhwanul Muslimiin nchini Misri, amelaani vikali kitendo cha kufukuliwa kaburi la sahaba wa Mtume Hujr bin Adi (RA) nchini Syria na kusisitiza kuwa, sahaba ni mtu anayetambuliwa na dini ya Kiislamu kuwa mtukufu, hivyo kufukua kaburi lake ni kuchezea matukufu ya dini ya Kiislamu. Aidha amesisitizia umuhimu wa kulindwa umoja wa umma wa Kiislamu kwa ajili ya kuzuia umwagaji damu na ukatili nchini Syria na kusema kuwa, hivi sasa taifa la Syria linakabiliwa na dhuluma na njama kubwa za maaduia wa Kiislamu na kwamba, Waislamu wanapaswa kuwa kitu kimoja dhidi ya njama hizo. Hivi karibuni kundi la kigaidi la Jab’hatunasra linalotekeleza vitendo vya mauaji dhidi ya raia wasio na hatia nchini Syria, lilifukua kaburi takatifu la Hujr bin Adi (RA) huko katika viunga vya mji mkuu wa Syria Damascus. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/palestina/item/31781-al-nusra-yakiri-kufanya-mashambulizi-600-huko-syria
AL NUSRA YAKIRI KUFANYA MASHAMBULIZI 600 SYRIA.