Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
imeandaa
kongamano la kimataifa la ‘Maulamaa na Mwamko wa Kiislamu’ ambalo litafanyika
Tehran wiki ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu Dk Ali Akbar Velayati amesema kuwa, kongamano
hilo ambalo litafanyika Jumatatu na Jumanne wiki ijayo litawaleta pamoja
Maulamaa 500 wa kigeni na 200 kutoka hapa nchini Iran.
Dk Velayati amesema, kongamano hilo
litachunguza matatizo ya nchi za Kiislamu na vile vile changamoto zilizopo
katika harakati za Mwamko wa Kiislamu. Aidha ameashiria njama za maadui za
kuibua vita vya kimadhehebu nchini Syria na kusema maadui wameanzisha njama
hizo baada ya kushindwa kuvunja muqawama nchini humo. Amesema maadui hao wa
Uislamu watafeli katika njama zao za kuibua vita vya kimadhehebu nchini Syria.
Velayati amesema, Iran inapinga harakati za Marekani na baadhi ya nchi za
Kiarabu na kieneo dhidi ya Syria. Amesema Iran inazihesabu njama hizo dhidi ya
Syria kuwa ni chuki na uadui dhidi ya Waislamu. Kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/31370-mkutano-wa-%E2%80%98maulamaa-na-mwamko-wa-kiislamu%E2%80%99-kufanyika-tehran