Kesho Maulana Sheikh Hemed Jalala,
Mwenyezi
Mungu akipenda atakuwa na msafara wa kuelekea nchini Iran, katika
msafara huo pia atakuwepo Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa
Salum, wakielekea katika kongamano la kimataifa la ‘Maulamaa
na Mwamko wa Kiislamu’, ambalo litafanyika Jumatatu na Jumanne,
Kongamano hilo litakuwa na Maulamaa 500 wa kigeni na 200 Maulamaa wa
Iran, kongamano hilo litachunguza matatizo ya nchi za Kiislamu na vile
vile changamoto zilizopo katika harakati za Mwamko wa Kiislamu.
Anaitajia dua zenu sana.