Bismillahir Rahmanir Rahim.
Laiti kama si mafuriko makubwa ya urafiki wa kweli na huruma iliyojaa na kumwagika ndani ya nafsi yake basi Imam Ali bin Abi Talib (a.s) asingechagua urafiki penye uadui. Kwa ajili hiyo wanahabari waaminifu kuanzia wafuasi wake hadi adui zake wamepokea kuwa: Pindi Zubayri na Talha walipong’ang’ania kumpiga vita, wakakataa kumtii huku wakimtuhumu katika tukio mashuhuri la vita vya ngamia (Jamal) Imam Ali bin Abi Talib (a.s) alikwenda akiwa hajajiandaa kwa vita, hana ngao wala silaha huku akiwaonyesha amani aliyodhamiria, kisha akanadi: “Ewe Zubayri! Njoo kwangu”. Zubayri akatoka akiwa amejiandaa kwa vita akiwa na silaha. Aisha alipomsikia Imam Ali bin Abi Talib (a.s) akipiga kelele akisema: “Ewe vita.”
Alipiga ukelele huo kwa kuwa kwa uchache alikuwa hana shaka kuwa hakuna kipingamizi isipokuwa ni Zubayri kuuawa, kwani anayepambana na Imam Ali bin Abi Talib (a.s) bila kizuizi huuawa hata kama atakuwa ni shujaa mkubwa wa namna yoyote ile au akawa na ujuzi wa juu wa kivita wa kiwango chochote kile.