NJIA ILIYONYOOKA..

Mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema: "Enyi watu, hakika mimi nawatangulia nanyi mtanikuta katika haudhi. Fahamuni kuwa mimi nitawauliza kuhusu vizito viwili, hivyo angalieni jinsi gani mtahusika navyo baada yangu. Hakika Mpole mtoa habari amenipa habari kuwa: Hakika hivyo viwili havitoachana mpaka vinikute. Nilimuomba Mola wangu hivyo na akanipa. Fahamuni hakika mimi nimewaachieni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Kizazi changu Ahlul-Bayt, hivyo msiwatangulie mtafarikiana, wala msiwaache mtaangamia na wala msiwafunze hakika wao ni wajuzi zaidi yenu. Enyi watu! Msiwe makafiri baada yangu ikawa baadhi yenu wanawauwa wengine hivyo mkanikuta huku mkiwa kundi dogo kama mfereji wa maji uliyoacha njia. Fahamuni kuwa Ali bin Abi Talib ni ndugu yangu na wasii wangu, atapigania Tafsiri ya Qur'an baada yangu kama nilivyopigania uteremkaji wake."

Rejea: Tarikh Yaaqubiy, Juz. 2 Uk. 109