Maulana Sheikh Hemed Jalala, Mudir wa Hawzat
Al-Imam Swaadiq (a.s), iliyopo Kigogo post, Jijini Dar es Salaam,
amewataka Waislam wote duniani kuikumbuka siku ya kifo cha Imam Hussein
(a.s), amesema Waislam wakitaka Uislam usichezewe duniani
na Maadui wa Uislam, Waislam hawanabudi kufuata nyayo za Imam Hussein
(a.s), nakukienzi kifo chake na kuyaenzi maneno yake Matukufu. Imam
Hussein (a.s) amesema: "Ikiwa dini hii ya Muhammad haiwezi kwenda mbele
isipokuwa kwa kufa mimi basi enyi panga nichukueni."
Waumini wa dini ya Kiislam wa Madhihabu mbalimbali
wakiwa Masjid Ghadiir Khum, Kigogo post, Jijini Dar es Salaam, kwa ajili
ya Kuomboleza kifo cha Imam Hussein (a.s), Mjukuu wa Bwana Mtume
Muhammad (s.a.w.w), aliyeuliwa kikatili na jeshi la Yazid ibn
Muawiyyah, katika Ardhi ya Karbala.
Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.