MAOMBOLEZO YA KIFO CHA IMAM HUSSEIN (A.S).


Maulana Sheikh Hemed Jalala, 
Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), Kigogo post, Dar es Salaam, akizungumzia tukio la Kihistoria juu ya kifo cha Imam Hussein (a.s).


 KUJIPIGA KIFUA ("MATAM").

Kitendo cha kujipiga kifua sio sehemu ya Imani, lakini ni njia ya kawaida sana ya mtu kuonyesha huzuni zake na upendo kwa mashahidi wa Karbala. Vitendo kama hivyo vimeruhusiwa katika "SHERIA" na vina fadhila kubwa,
kama inavyoelezwa katika tukio lifuatalo:

Katika vita vya Uhud, adui mmoja wa Uislamu aitwaye Utba Abi Waqas alimtupia jiwe Bwana Mtume (s.a.w.w), jiwe lile likampiga Mtume mdomoni, na jino moja au mawili yakang'oka, Uweis Qarani ambaye alikuwa mmoja wa Masahaba wa Bwana Mtume (s.a.w.w) anayeheshimiwa, na ambaye hakuwepo vitani alisikia tukio hili, alipatwa na huzuni mkubwa. Ili kuonyesha huzuni zake na upendo kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w), alichukua jiwe na akajipiga nalo na kung'oka meno yake ya mbele. Alikuwa hana hakika ni meno yapi aliyopoteza Mtume (s.a.w.w). Uweis akaamua kung'oa meno yote; alifanya hivyo. Wakati Bwana Mtume (s.a.w.w) aliposikia hili aliomba (DU'A), kwa ajili ya Uweis. Kama kitendo cha mtu kujiumiza mwenyewe na kutoa damu katika huzuni kwa ajili ya watu wa Mwenyezi Mungu ni vibaya, Mtume (s.a.w.w) angemlaumu Uweis na sio kumsifia.

Kupiga "MATAM" na kutoa damu katika jina la Imam Hussein (a.s) na Maimamu wengine ni kitendo che Thawabu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t).