WATAKAO ITAWALA DUNIA NI WATU WATANO.


Bismillahir Rahmanir Rahim.
Mwenyezi Mungu (s.w) anasema:

"Na wanakuuliza khabari za Dhul Qarnayn, sema: Nitakusomeeni baadhi ya hadithi yake."
(Qur'an: 18:83)

Dhul Qarnayn, ameitwa hivyo kwa sababu: Yeye amefika machweo ya jua na matokeo yake.

Imepokewa kutoka kwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) amesema: Dhul Qarnayn hakuwa Nabii wala hakuwa Malaika, lakini alikuwa mja mwema aliyempenda Mwenyezi Mungu, ndipo Mwenyezi Mungu (naye) akampenda.

Taz: Fat'hul bayan fyi maqasidil Qur'an  J.8 Uk.104

Watu walikwisha itawala dunia nzima ni wanne: Waumini wawili na Makafiri wawili, Ama Waumini ni Nabii Suleyman bin Daudi, na Iskandar (Dhul Qaynayn).

Ama Makafiri ni: Namruudh, na Bakhtansar. Na katika Umma huu, atakayeitawala dunia nzima ni: Imam Mahdi, ambaye jina lake kamili ni: Muhammad bin Hassan bin Ali bin Muhammad bin Ali bin Mussa bin Ja'afar bin Muhammad bin Ali bin Hussein bin Ali bin Abi Talib (a.s).

Taz: Fat'hul bayan fyi maqasidi Qur'an      J.8 Uk.105
       Tafsirul Qurtubi         J.8 Uk. 121

Ukitaka kujua matukio ya Adui wa Mwenyezi Mungu, Namruudh, basi soma:

Tarekh Ibn Athir    J.1 Uk. 115

Ukitaka kujua matukio ya Adui wa Mwenyezi Mungu, Bakhtansar, basi soma:

Tarekhut Tabari   J.1 Uk. 399

Na, ukitaka kujua matukio ya Dhul Qarnayn, soma:

Fat'hul bayan fyi maqasidi Qur'an        J.8 Uk. 103
Addurrul Manthur                           J.4 Uk. 436- 441