DHIMA YA DINI KWA WANAUME NA WANAWAKE.
Uislaamu ulipokuja uliwatwika dhima ya dini Wanaume na Wanawake. Na mtu wa kwanza kumwamini Mtume Muhammad (s.a.w.w), ni Mwanamke naye ni Bibi Khadija bint Khuwaylid (a.s). Aidha, Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume wake kuwa:
"Ewe Nabii! Watakapo kujia wanawake Waumini wanakuahadi ya kuwa: Hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawaua watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaozua wenyewe baina ya mikono yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana ahadi nao na uwatakie Maghfira kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa Maghfira, Mwenye kurehemu." Qur'an 60:12.