Bismillah Rahmanr Rahiim
Iliposemwa katika SUURATUL MAIDAH Aya ya 6 kuwa: " Enyi mlioamini! mnaposimama kwa (ajili ya) swala, basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu na miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba, basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni mchanga ulio safi na mpake nyuso zenu na mikono yenu Mwenyezi Mungu hapendi kukutieni katika taabu, lakini anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru". Mwenyezi Mungu anaagiza kuwa: Miguu ipakwe wala siyo kuoshwa. katika hali zote mbili itakavyosomeka Aya hii inafundisha kupaka si vinginevyo ukisoma: WAMSAH'UU BIRU UUSIKUM WA ARJULAKUM ikawa nasbu LAM katika ARJULA itakuwa mafuul ya IMSAH'UU. kwa sababu, RU-UUS iko katika mahallun nasba. Kanuni ya lugha ya Kiarabu inasema: "KULLU MAJRUU RIN LAFDHAN MANSUUBUN MAH'ALLAN" Na kama itasomwa LAM kwa ajarri ikawa ARJULI, basi itakuwa imefuata RU-UUS katika irabu yake. Kwa visomo vyote viwili kama tulivyovionyesha hapa, hukumu inabaki moja tu ya kupaka, hili ndio agizo la Mwenyezi Mungu.
Taz: Ruuhu Maany J. 6 uk. 115
Tafsrul Kabiir J. 11 uk. 161