GAIDI WA DAESH AKAMATWA NCHINI IRAN.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Kamanda wa jeshi la Iran katika mji wa Shahriar ametangaza kukamatwa kwa gaidi mmoja wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika sehemu ya Andisheh na amesisitiza kwa kusema kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh kilikuwa kinajipanga kwa kufanya matukio ya kigaidi ndani ya mwezi wa Muharram katika mji wa Teheran.
Hayo yamesemwa na kanali (Amini Yaminiy) alipokuwa amekutana na vyombo vya habari na kubainisha kuwa: mmoja kati ya magaidi wa Daesh tumemkamata sehemu iitwayo Andisheh katika mkoa wa Shahriar.
Aidha amebainisha kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh kilikuwa kimepanga kufanya mashambulio 300 ya kigaidi katika mwezi wa Muharram ndani ya mji mkuu wa Teheran, ambapo mpaka sasa tumepata ripoti nyingi kuhusu matukio hayo kupitia simu ya gaidi huyo na bado tunaendelea kumuhoji.