MAELFU YA WAIRAN WAJITOKEZA KATIKA MAZISHI YA MASHAHIDI.


















Maelfu ya wa Iran wamejitokeza katika mazishi ya Mashahidi waliokufa katika mashambulizi ya kigaidi.
Wiki iliyopita siku ya Jumatano jiji la Tehran lilikumbwa na mashambulizi kadhaa ya kigaidi. Watu kadhaa waliokuwa na silaha asubuhi ya jana waliingia katika majengo ya Bunge la Iran ambapo walikabiliwa na jibu kali la askari walinzi wa eneo hilo.
Watu kadhaa waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.
Sambamba na shambulizi hilo, magaidi wengine wanne walifyatua risasi ovyo katika haram ya Imam Khomeini kusini mwa jiji la Tehran ambako waliua mtu mmoja na kujeruhi wengine wanne. Gaidi mmoja alijilipua kwa bomu baada ya kukabiliwa na hujuma kali ya askari usalama, mwingine aliuuawa kwa kupigwa risasi, na gaidi mwenzao wa kike ametia nguvuni baada ya kujeruhiwa na askari usalama. Magaidi wengine kadhaa wametia nguvuni kabla ya kutekeleza uhalifu. Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuwa ndilo lililotekeleza mashambulizi hayo.