JENERAL QASSIM SOLEIMANI: MAREKANI HAINA NIA YA KUPAMBANA NA MAGAIDI WA DAESH.

Iraq na Iran zimekerwa na shutuma zilizotolewa na waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter ambaye amesema jeshi la Iraq halina ari ya kupambana na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la kigaidi la Daesh mjini Ramadi na kutekwa kwa mji huo wiki iliyopita na wanamgambo hao ni jambo ambalo lingeweza kuepukika.
Msemaji wa waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi amesema Carter ana taarifa zisiso sahihi na shutuma dhidi ya jeshi la nchi yake zimewashangaza huku Jenerali wa jeshi la mapinduzi la Iran
Qassim Solemaini akisema Marekani ndiyo isiyokuwa na ari ya kupambana na wanamgambo hao wa kundi la kigaidi la Daesh.
Marekani ilipeleka wataalam wake wa kijeshi zaidi ya 4000 kwa ajili ya kutoa mafunzo na ushauri wa kivita kwa jeshi la serikali la Iraq, ambapo kushindwa kwa jeshi hilo linalofundishwa na Marekani kunaashiria njama ya Marekani ya kutaka jeshi hilo lishindwe.
Jamhuri ya kiislamu ya Iran ilimtuma jenerali wake mmoja tu nchini Iraq ambaye ni jeneral wa jeshi la Quds anayefahamika kama Al-haj Qassim Soleiman, ambapo ameliandaa jeshi la mashia ambao kwa sasa ndio wanapambana wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh katika mji wa Ramad na wameshafanikiwa kuwazingira magaidi hao.
Jeshi la mashia linalofundishwa na jeshi la Iran limeweza kuwaangamiza wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh katika miji ya Anbal, Tikrit na Salahudin na kuweza kuikomboa miji hiyo kutoka mikononi mwa wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh.