Sheikh Hemed Jalala Kiongozi wa harakati ya Kiislam Medhehebu ya Shia
Ithna Ashariyyah Tanzania, leo amefanya ziara nyumbani kwa Mwanaharakati
mkongwe Sheikh Waziri Nyello aliyekuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Jumuiya
ya Shia Tanzania, taasisi ambayo inatambulika kwa jina la Tanzania
Ithna Ashariyyah Community (T.I.C), hivi sasa makao yake Makuu yapo
Kigogo Post, jijini Dar es Salaam. Sheikh Hemed Jalal na jopo la
Wanaharakati aliyoongozana nao katika ziara yake iliyofanyika leo
ilikuwa na lengo la kumjulia hali mwanaharakati huyo mkongwe baada ya
kusumbuliwa na maradhi ya Presha na Moyo yaliyopelekea kupumzishwa
hospitali kwa ajili ya matibabu hivi sasa hali yake inaendelea vizuri,
Sheikh Hemed Jalala aliongoza Dua maalumu kwa ajili ya kumuombea Sheikh
Waziri Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi katika maradhi yake.