MUGHIRA

Wale ambao hawashikamani na maagizo yao baada ya kupata ujuzi kuhusu dini; basi ili kuhalalisha tabia yao ya uzembe na kuonesha uovu wao katika mwanga bainifu, wananukuu Aya za Qur'an na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Hii ndio tofauti kati ya mwanachuoni wenye ujuzi na wasio na ujuzi; wasio na ujuzi hawawezi kunukuu Aya za Qur'an na Hadithi kuhalalisha makosa yao lakini wenye ujuzi wanajua namna ya kufanya hivyo.
Mfano wa hili katika historia ya Uislam ni Mughira bin Sheba. Alikuwa mtu mwenye elimu ya hali ya juu sana na alikuwa miongoni mwa washauri wa Makhalifa. Alifidiwa na kulipwa na serikali ya wakati huo kwa ajili ya ushauri wake. Wakati Ali (a.s) aliposhika madaraka kama Khalifa, Mughira alimshauri kwamba gavana wa Damascus (Mu'awiya) sio mtu mzuri, vilevile una uadui wa asili naye na tumetamani kwa muda mrefu kwamba lazima aondolewe kwenye nafasi hii ya ugavana. Alikuwa anamuomba Ali (a.s) kwamba kitu cha kwanza anachopaswa kufanya ni kumuondoa gavana wa Damascus. Imam Ali (a.s) akasema kwamba hii ilikuwa ndio nia yangu kuanzia mwanzo bila kujali ushauri wako, lakini sikusudii kufanya hili kwa sababu uliyonayo katika akili yako, sababu niliyonayo akilini mwangu ni tofauti.
Hivyo kwa kuwa kwake Khalifa, Amirul-Mu'minin (a.s) alitoa amri yake ya kwanza kumuondoa gavana wa Damascus katika nafasi hiyo. Yeye (a.s) alisema kwamba katika serikali yangu mtu mkandamizaji hawezi kubaki katika wadhifa wa serikali hata kwa siku moja.
Baada ya muda kidogo mshauri huyu (Mughira) alikuja tena na kumpa ushauri mwingine. Alimuambia Ali (a.s) kwamba kwa mtazamo wa kisiasa hukufanya kitu sahihi. Hii ni kwa sababu nafasi yako kama Khalifa bado haijathibitika vizuri katika mji wa makao makuu ya serikali, hivi karibuni yalitokea mauaji ya Khalifa wa tatu na kuna mgogoro katika mji wa Madina - hali ya ghasia na machafuko kila sehemu. Chini ya mazingira haya, kwanza ungeimarisha makao makuu na kisha ndipo ukamkabili mtu mwingine, lakini bila kuzingatia hili umeanza mapambano na gavana, tena wa eneo kama Damascus. Hii sio hatua nzuri ya kisiasa. Ndani ya muda wa siku chache mshauri huyu wa serikali alitoa ushauri wa aina mbili tofauti, kabla ya gavana kuondolewa alishauri kwamba gavana huyu lazima aondolewe mara moja, lakini baada ya gavana huyu kuondolewa mara moja aligeuza ushauri wake na akasema kwamba hatua hii haikupaswa kuchukuliwa.

Siku moja mshauri huyu alizozana na Ammar (r.a). Ammar (r.a) aliingia kwenye mapamabano naye wakati wanabishana juu ya suala fulani. Wakati Ali (a.s) alipata habari kwamba Ammar (r.a) anabishana na Mughira, Yeye (a.s) alimuita Ammar na akasema 'Ewe Ammar! Achana naye, usibishane naye, na usiwe na mazungumzo yoyote naye au kujadiliana naye.' Ammar (r.a) akasema: 'Ewe Amirul-Mu'minin, anasoma hadithi za Mtume (s.a.w.w) na kusimulia matendo ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w). Anawapotosha watu kwa kusoma Aya za Qur'an na hivyo ni wajibu kwangu mimi kuhojiana naye.' Ali (a.s) alisema: 'Ammar achana naye. Anaelewa tafsiri ya Aya za Qur'an, ni mjuzi wa hadithi na matendo ya Mtume (s.a.w.w), ni hafidhi wa Qur'an, na anaelewa sheria za dini kwa ajili ya matendo ya ibada, lakini ametumia Qur'an, hadithi, dini na sheria zake kama njia ya kuthibitisha na kuhalalisha makosa yake. Hii ndio njia anayotumia kuondokana na hatia, makosa na majukumu yake.
'Wakati Imam Ali (a.s) alipomsikia Ammar bin Yasir anabishana na Mughira, Yeye (a.s) alimuambia Ammar achana naye. Kwa sababu amechukuwa tu aina ile ya dini ambayo humleta karibu na dunia yake hii na kwa makusudi amejiingiza kwenye hali ya mashaka ili aweze kutumia shaka hizi kama njia ya kuhalalisha anasa zake.'
Rejea: Nahjul Balagha, semi ya 405
Na Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi