IMAM KHOMEIN (R.A)

Mfumo wa Wilayah unakataa udhalili.

Tuangalie jinsi gani Imam Khomein (R.A) alivyokumbwa na misukosuko huko katika ardhi ya Iraq.
Mnamo tarehe 24/09/1978 vikosi vya Iraq vilizingira nyumba ya Imam Khomein (R.A) huko Najaf tukufu na kumpa sharti kuwa ili aendelee kubaki Iraq ni lazima asimamishe harakati zake za kisiasa, atangaze waziwazi kuwa ameacha mapambano, lakini Imam aliendelea na mapambano. Hapa ni muhimu kukumbuka kauli ya Imam Hussein (a.s) "DAIMA UDHALILI NI MWIKO KWETU" hii ndio kauli iliyombakiza Imam Khomein (R.A) katika uwanja wa mapambano na kufikia daraja la mafanikio, leo hii ni hajabu kwetu kuona watu wananyenyekea watawala dhalmu na kuacha mafundisho matukufu ya Uislam. Nijukumu la kila mmoja wetu kupambana na Mayazid wazama zetu za leo katika ardhi zetu.

"KUPINGA MFUMO WA WILAYAH NI SAWA NA KUUNGA MKONO UTAWALA HARAMU WA ISRAEL.” Imam Khomein (R.A) anasema “Matatizo yetu yote yanatokana na Israel na Marekani nayo ni sehemu ya Israel.”