Waumini wa dini ya Kiislam Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah wameungana
na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kufanya dua maalumu kumuombea
Shahidi Sheikh Abdul Qadir (Doktoor Abdul Qadir) aliyeuawa kwa kupigwa
risasi Uganda alipokuwa akitokea Msikitini, dua hiyo ilifanyika katika
Msikiti wa Khoja Shia Ithna Ashariyyah uliyopo Posta, Dar es Salaam
kabla ya kisomo cha dua ilisomwa historia ya maisha ya Shahidi Sheikh
Abdul Qadir na Sheikh Ramadhani Kwezi kutoka Bilal Muslim Mission
Tanzania kukifuatiwa na wazungumzaji mbalimbali, Sheikh Jabir Chandoo
alizungumzia juu ya umuhimu wa ufanyaji Tabligh huku akisisitiza umuhimu
wa kuwa na mshikamano katika kufikisha ujumbe wa Ahlul Bayt (a.s),
Kiongozi wa Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa kilichopo Upanga, Dar es
Salaam Sayyid Shahidi alisema ni muhimu kuwa na tahadhari sana hivi sasa
maadui wameanza kazi katika nchi zetu mwisho Imam wa Masjid Al Ghadir,
Kigogo Post Sheikh Hemed Jalala alisoma Majilisi ya Imam Hussein (a.s)
kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Shahidi Sheikh Abdul Qadir. "Hakika
sisi sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea."