Imam Muhammad Baqir (a.s) alizaliwa siku ya Ijumaa tarehe 1 Rajab mwaka mwaka wa 57 HIjiriya, miaka saba baada ya kifo cha Imam Hassan Al-Mujtaba (a.s), wakati Imam Hussein (a.s) alipokuwa akipitisha maisha yake kimya kimya na wakati ambao muda ulikuwa ukiendelea kuzaa sababu za masaibu ya Karbala. Wakati huu ulikuwa mgumu sana kwa marafiki wa Dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na wafuasi wa Hadhrat Ali bin Abi Talib (a.s) waliokuwa wakiwindwa ili wakatwe vichwa vyao au wasulubiwe. Kuzaliwa kwa mtoto huyu kulikuwa katika muda huu wa mfululizo wa matukio yalioongozana kwenye masaibu ya Karbala.  
Mwenyezi Mungu anasema:
“Siku tutakapowaita kila watu pamoja na viongozi (Imam) wao, basi atakayepewa kitabu chake cha amali kwa mkono wa kulia, hao watavisoma vitabu vyao kwa furaha.”
(Qur’an: 17:71)
Mtukufu Mtume (s.a.w.w) anasema:
“Ye yote yule afaye pasina kumjua Imam wa zama zake, atakuwa kafa kifo cha ujinga.”