WAUMINI WA MADHEHEBU YA SUNNI, WAMEUNGANA NA WAISLAM WENZAO KATIKA SHEREHE YA MAZAZI YA MTUKUFU MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W).


Waislamu wa Madhehebu ya Sunni wameungana na Waumini wa Madhehebu nyingine leo katika Sherehe ya Maulid ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), Maulid hayo yamefanyika Posta jijini Dar es Salaam.

Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia rehema Mtume, na Malaika wake wanamteremshia rehema Mtume, enyi mlioamini! Muombeni rehema (Mtume) na muombeni amani". 33:56 iliposemwa Aya hii, Maswahaba waliuliza Mtume: Watamuombeaje rehema? Mtume akawafundisha, semeni: Allahumma swali a'laa Muhammad wa Aali Muhammad. Hili ni muhimu sana kuliewa, kwa sababu, wako watu wengi wanapomuombea rehema Mtume husema: Swallallahu Alayhi wasallama. Hili ni kosa kubwa kabisa, kwa sababu Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) hakufundisha hivyo. Bali amesisitiza akisema: "Msiniombee rehema kwa kunikata, mkisema: Allahumma swali A'laa Muhammad, mna nyamaza, lakini semeni: Allahumma swali A'laa Muhammad wa Aali Muhammad.

Rejea: Yanabiiul Mawadda J. 1 uk. 6