Hassan Rohani mgombea uchaguzi wa rais wa Iran amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi ujao hapa nchini ili kuleta hamasa ya kisiasa. Rohani amesema hayo katika kampeni zake za uchaguzi kwenye mkoa wa Gilan na kuongeza kwamba, kujitokeza kwa wingi wananchi kunahitajika ili kuleta hamasa ya kisiasa hapo Juni 14, na pia kuisaidia nchi kukabiliana na umasikini, ughali wa maisha na ukosefu wa ajira.
Rohani aidha amesema, matatizo ya hivi sasa ya nchi yanaweza kutatuliwa kwa kuimarishwa umoja na mshikamano wa wananchi.
Wakati huo huo mgombea mwingine wa uchaguzi huo Saeed Jalili amebainisha umuhimu wa kulinda ardhi yote ya Iran na kusema kuwa Tehran haitofanya mazungumzo na nchi yoyote kuhusiana na umuliki wake wa visiwa vitatu vilivyoko katika Ghuba ya Uajemi vya Abu Musa, Tunb Kubwa na Tunb Ndogo.