Bismillahir Rahmanir Rahim.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Katika nyumba ambazo
Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, humtukuza humo
asubuhi na jioni.” Qur’an: 24:36
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik anasema: Aliposoma Mtume
Aya “Fyi buyuutin adhinallahu antu fa’a” anamaanisha, “Katika nyumba ambazo
Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe.”
Mtu mmoja akamsimamia akasema: Ni nyumba gani hizi ewe Ntume
wa Mwenyezi Mungu? Mtume akajibu: Ni nyumba za Mtume, mara Abubakr akamsimamia akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!
Nyumba hii ni miongoni mwa hizo? Akaonyesha nyumba ya Ali na Fatma (a.s) Mtume
akajibu: Ndiyo, ni miongoni mwa nyumba zenye kutukuzwa.
Rejea: Addurrul Manthur J.5 Uk. 91
Alburhan fyitafsiri Qur’an J.3 Uk. 138
Tafsirus Saafi
J.3 Uk. 437
Ruuhul Maany J.18 Uk. 255
Almizan fytafsiril Qur’an J.15 Uk. 153
IJUMAA KAREEM