WAFUASI WA IMAM ALI BIN ABI TALIB (A.S) WATAFUZU SIKU YA KIYAMA.

Bismillahir Rahmanir Rahim.
 

Iliposemwa: "Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe." (Qur'an: 98:7)

Imepokewa kutoka kwa Jaabir bin Abdillah anasema: Tulikuwa tumeketi pamoja na Mtume (s.a.w.w) mara akatokea Ali bin Abi Talib, Mtume (s.a.w.w) akasema: "Ninaapa kwa ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hakika huyu (Ali) na Shia (Wafusi) wake lazima ni wenye kufaulu siku ya Kiyama. "Pale pele Mwenyezi Mungu akatemsha Aya hii. 98:7.

Taz: Tafsirut Tabari    J. 30 Uk 171
Addurrul Manthur       J. 6 Uk. 643
Tafsirus Saafi            J. 5 Uk. 355
Alburhan fyitafsiril Qur'an   J. 4 Uk. 491
Almizan fyitafsiril Qur'an    J. 20 Uk. 482

SIFA ZA MASHIA ITHNA ASHARIYYAH

Iliposemwa: "Shia (wafuasi) wa Ali watafaulu siku ya Kiyama." Ni nani Shia? Kwa kujibu swali hili, ni lazima kuwarejea mabingwa wa lugha ya Kiarabu kama ifuatavyo:

1- Amesema Ibn Mandhuuri kuwa: Shia ni, watu ambao waliokusanyikia jambo fulani.
2- Az-Zujaaj anasema: Shia ni, wafuasi wa Mtu.
3- Anasema Al-Az-hary kuwa: Shia ni, watu wanaowapenda kizazi cha Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Taz: Taajul Aruusi   J. 21 Uk. 302 - 303
Lisanul Arabi          J. 7 Uk. 258

Tamko la Shia katika Qur'an limetumiwa kwa maana zifuatazo:

1- Maana ya Kundi 6:65, 6:159, 15:10, 28:4, 30:32, 37:83.
2- Maana ya Jamaa / Ansaar 28:15, 32:54. 54:51
3- Maana ya Taifa 19:69
4- Maana ya Kuenea 24:19
5- Maana ya Adui 28:15

Mbegu ya Shia imepandwa katika shamba la Islam na yeye mwenyewe Mtume wa Islam na Waislamu. Alipowaambia Maswahaba wake juu ya Ali bin Abi Talib (a.s): "Naapa kwa ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hakika huyu (Ali) na Shia wake lazima ni wenye kufaulu siku ya Kiyama." Palepale Mwenyezi Mungu akateremsha Aya ya saba ya Suratul bayyinah.

Hawa wafuatao ndio Shia waliotajwa katika Aya iliyotangulia hapo juu, ambao sifa zao ni hizi zifuatazo:

Imepokewa kutoka kwa Imam Abul Hasan Ar-Ridha (a.s) amesema: "Shia  wetu ni yule mwenye kufuata mambo yetu, anayechukua maneno yetu, anayeachana na maadui maadui zetu, na yeyote asiye na sifa hizo basi si katika sisi."

Amesema Imam Jaafar As-Saadiq (a.s) "Ni muongo yule anayedai kuwa yeye ni katika Mashia wetu, naye anashikamana na kishikio kisichokuwa chetu."

Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Abbas anasema: Amesema Mtume (s.a.w.w): "Anayependa kushikamana na kishiko imara kisichovunjika, basi ashikamane na Wilaya ya Wasii wangu Ali bin Abi Talib (a.s).

Taz: Tafsirus Saafi      J. 1 Uk. 284
Alburahan fy tafsiril Qur'an J. 1 Uk. 536

Amesema Imam Jaafar As-Saadiq (a.s): "Naaswib (adui wa Ahlul - Bayt) siyo yule anayetuchukia sisi Ahlul - Bayt (a.s) kwa sababu, wewe humpati yeyote anayesema kuwa: Mimi ninamchukia Muhammad na watu wa Nyumbani kwake, lakini, Naaswib ni yule anayekuchukieni nyinyi, naye anajua kuwa nyinyi mnatutawalisha sisi, na mnajitenga mbali na maadui zetu. Mwenye kushibisha adui yetu, basi hakika amemuuwa Walii wetu."

Anasema Imam Abu Hasan Ar-Ridha (a.s) kuwa: "Mwenye kuwapiga vita Shia (wafuasi) wetu, bila shaka ametupiga vita sisi. Na anayewaunga (kushikamana nao) bila shaka ametuunga sisi, kwa sababu wao wanatokana nasi, wameumbwa kwa udongo wetu. Anayewapenda, basi huyo ni katika sisi, na ayewachukia basi huyo si katika sisi."

Imepokewa kutoka kwa Hamiiry amesema: "Siku moja Imam Ali (a.s) alitoka akatukuta tumekusanyika akasema: "Nyinyi ni akina nani? Na limekukusanyeni jambo gani? Tukajibu: Sisi ni Shia (wafuasi) wako ewe Amiirul Muuminiina! Akasema: Mbona sioni alama zenu za Ushia? Tukauliza Alama za Ushia ni zipi? Akasema: Nyuso za manjano kwa ajili ya Swala za usiku, kudhoofu macho kwa ajili ya kumuogopa Mwenyezi Mungu, kunyauka midomo kwa ajili ya Swaumu, waliogubikwa na Alama za unyenyekevu."

Amesema Imam Jaafar As-Saadiq (a.s): "Si Shia (mfuasi) wetu anayesema kwa Ulimi wake na akapingana na matendo yetu na nyendo zetu, lakini, Shia wetu ni yule anayefanana nasi kwa Ulimi weke na Moyo wake, kisha akafuata nyendo zetu na kutenda matendo yetu, hao ndiyo Shia wetu."

Akasema Imam Jaafar As-Saadiq (a.s) kumwambia Shia wake Ali bin Abdil Azizi: "Kisikuhadae kilio chao, kwa sababu, Taq-wa imo moyoni."

Taz: Biharul An-waar       J. 15 Uk. 265 - 290
Swifaatush Shia                      Uk. 10 - 31

Hawa ndio Mashia watakaofuzu siku ya Kiyama ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameteremsha Aya ya saba ya Suratul bayyina kwa kusema: "Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe." Na bwana Mtume (s.a.w.w) akasema: "Naapa kwa ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake hakika huyu (Ali) na Shia wake, lazima ni wenye kufaulu siku ya Kiyama." Mashia wasemwao hapa ni wale wenye sifa zilizoonyeshwa hapo juu.

MAKUNDI MAWILI YA WAISLAMU.

Inasemekana Mtume (s.a.w.w) amesema: "Hakika mwanangu huyu (Hassan bin Ali) ni bwana, na huenda Mwenyezi Mungu akapatanisha kwa ajili yake makundi mawili makubwa ya Waislamu."

Taz: Nabiyyi lil Hasan bin Ali (a.s)
Sahihi Bukhari, kitabus sulhi, babu qawlin

Makundi mawili ya Waislamu, ambayo yanatarajiwa kupatana kwa ajili ya Imam Hasan bin Ali ni:

1- Kundi la Imam Hasan (a.s).
2- Kundi la Muawiyyah.

Ni nani Hasan? Yeye ni: Hassan bin Ali Abi Talib bin Abdil Muttalib bin Hashimi.
Mama yake ni: Fatma bint Muhammad bin Abdillahi bin Abdil Muttalib bin Hashimi.

Na, nani Muawiyyah? Yeye ni: Muawiyyah bin Abi Sufyan bin Umayya bin Abdi Shamsin.
Mama yake ni: Hindu bint Utba.

Mtume (s.a.w.w) anasema: "Kila umma unayo maafa makubwa, na maafa makubwa ya umma huu ni banu Umayya."

"Mti (ukoo), ulio laaniwa katika Qur'an, ni banu Umayya."

Taz: Kanzul Ummal    J. 11 hadithi Na. 31755
Tafsirul Qurtubi           J. 10 Uk. 286
Addurrul Manthur        J. 4 Uk. 346