MAELEZO JUU YA DUA
AL-IFTITAH:
Dua
al-Iftitah ilifundishwa na Imam wetu wa kumi na mbili (A.S) kwa ajili ya Mashia
kusoma kila usiku wa mwezi wa Ramadhani. Dua hii ni bora sana kwa ajili ya
kujenga mwelekeo mzuri wa mwanadamu kwa Mola wake kwa vile inazungumzia
vipengele vingi vya udhaifu wa binadamu na neema za Allah. Dua hii inaweza
kugawanyika sehemu mbili:
Uhusiano
wa binadamu na Mwenyezi Mungu.
Viongozi
wa ki-Ungu watakatifu.
Sehemu
ya kwanza ya Dua hii inaelezea sifa mbalimbali za Mwenyezi Mungu, na
inadhihirisha hali ya huruma na upendo wa Mwenyezi Mungu juu ya mwanadamu.
Sehemu hii ya Dua inaweza kugawanyika zaidi katika vifungu vifuatavyo:
KUMTUKUZA
MWENYEZI MUNGU: Kama ilivyo taratibu ya Dua, Dua hii ya al-Iftitah inaanza na
kumsifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Hii sio kwa sababu kwamba Mwenyezi Mungu
anahitaji kusifiwa kabla ya yeye kujibu Dua zetu, bali ni kumkumbusha mwombaji
juu ya Mweza wa yote anayeongea naye, na hatimaye kuweka hofu juu ya Allah
katika nyoyo ambayo mara nyingi zinakuwa hazizingatii.
Uanzaji
wa Dua hii unamuweka muombaji katikati ya matumaini na hofu, mtazamo bora
wakati unapoomba. Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa huruma, lakini pia ni mkali wa
kuadhibu. Binadamu wasiwe wenye kukata tamaa, wala wasijiamini sana bali wadumu
katika njia yake.
MSISITIZO
JUU YA UPWEKE (TAWHIID) WA ALLAH: Mwenyezi Mungu hana mshirika wala mtoto, na
anayo mamlaka kamili na udhibiti usiogawanyika juu ya viumbe. Wakazi wa angani
na mbiguni wanamtegemea yeye. Hii ni kuimarisha utegemeaji wa muombaji juu ya
Mwenyezi Mungu, kwani hakuna mwengine tena anayeweza kumgeukia.
UKARIMU
WA MWENYEZI MUNGU: Hazina ya Mwenyezi Mungu hazifilisiki wala haziishi, na
wakati wote zinatolewa kwa ukarimu juu ya viumbe wake. Shida za binadamu ni
nyingi mno, na kwa kuuwacha wazi mlango wa Dua, Mwenyezi Mungu amewapa ufunguo
wa kwenye hazina zake. Milango yake wakati wote iko wazi, na hakuna muombi
yoyote kwake yanayokataliwa bila ya majibu fulani.
Lakini
mara nyingi mwanadamu ni mtovu wa shukurani, ana wakati wote ni mlafi.
Anategemea kwamba Dua zake siku zote zitajibiwa mara moja. Wakati kuridhika
kama huko hakupatikani, yeye anageuka, badala ya kujikumbusha yeye mwenyewe juu
ya neema zote anazozifaidi.
MAHUSIANO
KATI YA ALLAH NA MWANADAMU: Ni uhusiano wa ajabu kweli kweli! Ingawa ni
mwanadamu anayemhitaji Allah, na anapaswa kujitahidi kumuelekea yeye; ni
Mwenyezi Mungu anayemualika na kumhimiza yeye kuja, ambaye anaonyesha upendo na
huruma na anaendelea kumpendelea kwa njia nyingi. Kama anavyosema Imam wa nne
katika Dua Abu Hamza Shimali: "Shukurani zimwendee Allah ambaye huniitikia
mimi pale ninapomwita, ingawa mimi ninasitasita pale anaponiita, na sifa ni kwa
juu yake Allah ambaye hunipa mimi wakati ninapomuomba, ingawa mimi ni bakhili
pale anaponiomba." Hii inafaa kuitafakari kwa wale wanaomdhania Mwenyezi
Mungu kwamba ni bwana wa kidhalimu anayeweka sheria juu ya wanadamu.
Sehemu
hii ya Dua ni somo bora sana katika mtazamo wa Kiislam wa sifa za Mwenyezi
Mungu. Mola wa Uislam ni mwenye upendo, Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma
anayewatendea wanadamu kwa ubora zaidi kuliko wanavyostahili. Msingi wa
uhusiano kati ya Mwenyezi Mungu na mwanadamu ni upendo wa Muumba juu ya viumbe
wake. Ni juu ya mwanadamu kuupekua moyo wake kwa ajili ya mwitiko wa
kutendeana.
Sehemu
ya pili ya Dua hii inamtakia rehema na amani Mtume Mohammad (s.a.w.w) na
Ma'asuumin wote, na halafu inazungumzia jukumu la Imam wa kumi na mbili (A.S).
KUMSWALIA
MTUME MOHAMMAD S.A.W.W (SALAWAT): Baada ya imani juu ya Mwenyezi Mungu, sehemu
muhimu ya dini inayofuata ni imani juu ya wale aliowatuma. Hivyo baada ya
kukiri Ukuu na Upole wa Muumba, Dua hii inatufundisha sisi kuwakiri wale
viongozi wa Ki-Ungu watukufu kama viongozi wetu kuelekea kwa Allah (s.w.t)
Rehema na amani zinatumwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kama ishara ya mapenzi na
shukurani kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na kutambua kwamba yeye ni binadamu na
anahitaji huruma na neema kutoka kwa Allah. Inaimarisha vilevile ukumbusho kwa
Mtume (s.a.w.w) na msukumo wa kuifuata njia yake.
REHEMA
NA AMANI JUU YA MA'SUMIIN: Baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) warithi waandamizi
wake wanakumbukwa na kuombewa. Hawa ndio viongozi halisi wa Umma wa Kiislam
ambao waliteuliwa na Mwenyezi Mungu. Imani juu yao, na upendo kwao ni sehemu
muhimu ya imani ya Kishia.
JUKUMU
LA IMAM WA KUMI NA MBILI (A.S): Katika kila zama Mwenyezi Mungu huwa anaye
mwakilishi wake ambaye anamwongoza viumbe wake kwenye kusimamisha haki na
uadilifu katika ardhi. Huyo Imam wa kumi na mbili ndiye kiongozi wa zama zetu
hizi, amabaye atakuja kudhihiri na dini ya Mwanyezi Mungu itashinda (dini zote)
duniani.
Sehemu
ya mwisho ya Dua al-Iftitah inazungumzia kuhusu kuja kwake kuwaandaa waumini
juu ya kusimama kwa utawa wa Allah unaotarajiwa juu ya ardhi. Kuomba msaada na
ushindi kwa ajili ya Imam wa kumi na mbili (Imam Mahd) kutukumbusha sisi kwamba
tunamngojea yeye, na tunahitaji kujiandaa kwa ajili ya kuja kwake. Tunakuwa
tunatambua wajibu wetu katika wakati wa kughibu (kufichika) kwake, na umuhimu
wa kujifundisha sisi wenyewe kama wasaidizi wake. Tunaomba kwa ajili ya ndoto
ya mwisho ya Muislam, dini ya Mwenyezi Mungu inapata umuhimu mkubwa, na ukafiri
na unafiki vinadhalilishwa.
Dua
al-Iftitah inatukumbusha sisi kwamba imani na vitendo vyote ni muhimu na vya
lazima ili kuwa muumini halisi na wa kweli. Imani juu ya Mwenyezi Mungu
inafungamana na kuufanyia kazi ujumbe wake uliokuja na Mtume wake, na
kusimamisha dini yake duniani. Wakati ambapo hilo linaweza kufanyika tu kupitia
kwa Imam, sisi tunapaswa kufanya kazi na kuomba kwa ajili ya kudhihiri kwake.
Wanadamu wanaweza kufaidi uadilifu na amani halisi, na kutimizwa kwa haja zao,
chini ya kiongozi huyo Mtukufu.
Dua
al-Iftitah sio maombi tu kwa ajili ya shida na haja zetu, bali ni ufundishaji
wa mizizi ya iman, na upangaji kwa ajili ya namna ya maisha. Inabakia kwetu
sisi kuandaa jedwali la maisha yetu wakati tunaposoma Dua hii katika kila usiku
wa Ramadhani.