IMAM HUSSAIN (A.S) ANA NAFASI GANI MBELE YA MWENYEZI MUNGU (S.W.T).?

                                                                                                     Ashura ndani ya Nigeria- Muharram

Imam Hussein (a.s) ana nafasi maalumu mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Hii ni kwa sababu alitoa kila kitu alichokuwa nacho kwa ajili ya kuunusuru Uislamu katika wakati ambao hakuna aliyeweza kufanya hivyo. Muhanga wa Imam Hussein (a.s) una somo kubwa ndani yake, kwamba uliwaokoa Waislamu wa zama zote kutokana na kupotezwa na watu waovu. Hivyo ukumbusho wa Imam Hussein (a.s) una nafasi maalum katika Uislamu. Njia zote ambazo Waislamu wanazitumia leo katika kuziweka hai kumbu kumbu za Imam Hussein (a.s), hufanya kwa mujibu wa sheria. Maadui wa Uislamu wanaogopa kwamba, kwa kumkumbuka Imam Hussein (a.s), Waislamu kamwe hawatapotoshwa. Kwa hiyo juhudi zote zifanywe ili kuwazuia watu kutokana na kumkumbuka Imam Hussein (a.s). Maadui wa Uislamu wanatutaka sisi tuamini kwamba wao ni Waislamu wazuri sana, na kisha wanatuambia kwamba ukumbusho wa Imam Hussein ni “BIDAA” (Kitu kilichozushwa ambacho hakikufanywa na Mtume). Ukumbusho wa Imam Hussein (a.s) hupo juu ya “Sunnah” na “Sirah” ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w). Ni nguvu inayotoa uhai kwenye Uislamu na kwa hiyo ni kitendo chenye “Thawabu” kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t).

                                                                                                       Ashura ndani ya Karbala- Muharram