Maulana Hemed Jalala Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), amesema lengo la Darasa la Ujue Ushia lililopo Ilala Sharifu Shamba Jijini Dar-es-Salaam sijingine bali nikutaka kuifumbua macho jamii ya Kiislamu kuwa Ushia si Uhindi bali umeazishwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w), pia amewataka Waislamu kuudhulia kwa wingi katika Darasa hilo iliwapate faida bila ya kutazama utofauti wa Madhehebu yao, mwisho amemalizia kwa kunukuu maneno ya Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhimu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa: “ Tunaposhajiisha suala la umoja, madhumuni yetu sio kumtaka Sunni awe Shia au Shia awe Sunni au Muislamu wa madhehebu fulani aache madhehebu yake na kufuata madhehebu nyingine, la hasha, umoja tunaoukusudia ni kuwa na msimamo mmoja na kutoruhusu maadui watumie hitilafu zetu ndogo za kimadhehebu kwa ajili ya kutufarakanisha.